Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewahakikishia Watanzania mbele ya Rais Samia leo kwamba hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa kwakuwa Serikali ina chakula cha kutosha.
Akiongea mbele ya Rais Samia aliposimama kuwasalimia Wananchi wa Kondoa, Dodoma akiwa njani kwenda Manyara, Bashe amesema “Niwahakikishie Watanzania hakuna Mtanzania atakufanya kwa njaa, Serikali ina chakula cha kutosha na hivi sasa kupitia Wizara, Halmashauri zinaonesha na kutuletea taarifa, pale ambapo bei ya mahindi inakuwa imepanda sana Serikali inapeleka chakula na kuuza kwa bei ya chini ili Wananchi waweze kununua “
“Mpaka sasa Mh. Rais, Halmashauri 41 tumeshazipelekea chakula na sisi kama Serikali tunafungua duka chini ya maelekezo ya Halmashauri tunauza vyakula kwa Mwananchi mmojammoja kwa bei ya chini sio kuwauzia Wafanyabiashara”
“Nimalizie kuwaambia Wakulima, kama hatutofanya mabadiliko katika Sekta ya Kilimo kipindi hiki, tusahau, tuna Rais ambaye ana utashi wa kisiasa na ana utayari wa kuweka fedha ili kuondoa matatizo yetu, bajeti imekwenda karibu Bilioni 900”