Katika kukuza sekta ya Kilimo na kuwaisaidia wakulima nchini, Serikali imeombwa kuweka kifurushi maalum cha Kilimo kitakachohusisha Mbolea, Dawa na Mbegu.
“Unaweza kumsaidia mkulima kwenye mbolea lakini dawa na viuwatilifu ni kufuru unaweza kuambiwa leo bei ni Laki Mbili na Thelathini lakini baada ya wiki moja ukaigusa hiyo dawa unaambiwa Laki Mbili na Themanini,” ameyasema hayo Dick Lukala ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Dick Lukala.
“Kama unamsaidia mkulima kwenye mbolea lakini kwenye dawa bei yake haeieleweki, hivyo shida tuwe na kifurushi cha ruzuku ili vitu vyote Mkulima avipate kwa bei elekezi,” amesema Lukala.