Mkuu wa Mkoa wa Geita , Martine Shigela ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Geita kuhakikisha wanafanya vikao mara kwa mara na wachimbaji wadogo wa Madini katika Mkoa huo lengo likiwa ni kutatua changamoto mbalimbali zitokanazo na wao kushindwa kulipa kodi.
“Nafahamu kwamba kwenye Mkoa wetu wa Geita tunayo changamoto na changamoto inatokana na Base ya uchumi wa Mkoa Base ya sekta ya Madini nilikuwa naongea na meneja wetu hapa ishu ya Mlipa kodi hasa wachimbaji wadogo ukikaa nao ukiwasikiliza wanakwambia sisi tunapata shida na TRA unauliza shida gani si mnalipa pale kwenye soko wanasema sisi hatulipi kwenye soko , “ Mkuu wa Mkoa wa Geita.