WADAU wa ufugaji wa kuku nchini wameonesha imani kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kusaidia kulinda soko la ndani la uzalishaji wa vifaranga.
Wakizungumza katika mdahalo ulioshirikisha wazalishaji wa vifaranga wa ndani ya nchi mawakala wa uuzaji wa vifaranga pamoja na wafugaji, kwa pamoja wadau hao walieleza kuwa uingizwaji wa vifaranga hivyo umekuwa na athari kiuchumi.
Akizungumzia uingizwaji huo wa vifaranga Mkurugenzi wa Kampuni ya Organia inayozalisha vifaranga hapa nchini, Albert Momdjian alibainisha kuwa kumekuwa na wimbi la uingizwaji wa vifaranga kwa njia zisizokuwa za halali kutoka nchi jirani hususan Kenya na Malawi ambavyo huuzwa sokoni kwa bei rahisi.
Alisema,” vifaranga vinavyoingizwa nchini hasa vile vua njia zisizokuwa halali vimekuwa na athari kubwa kwa wazalishaji wa vifaranga wa ndani hasa kutokana na kuleta ushindani usiokuwa sahihi, wao wanaweza uza hata kwa bei ya chini sababu hawaingia gharama za kodi katika kuingiza.”
“Ni imani yangu kuwa chini ya serikali ya Rais Samia kila kitu kinaenda kuwa sawa hasa wahusika watachukuliwa hatua kwa kuwa wapo wanaoingiza kwa njia ya mabasi huku wengine wakiuza hadharani iwe eneo la Tazara na kwengineko” aliongeza Momdjia.
Pia alisema kuwa kwa kampuni zinazopewa vibali vya kuagiza vifaranga nje ya nchi na zenyewe zinatakiwa kudhibitiwa kwa kuwa zipo nchi kama Marekani na nyingine za ulaya zilijikuta zikiingiza magonjwa kwenye nchi zao kutokana na kuruhusu vifaranga kutoka nje ya nchi zao ambavyo vilikuwa na magonjwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji wa Kuku Tanazania (TABROFA) Costa Mrema alibaisha kuwa kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya watanzania kujiajili kwenye ufugaji wa kuku, ni vema suala la kuingizwa kwa vifaranga vya nje likaangaiwa kwa umakini zaidi.
Alisema “sera ya nzuri ya Rais Samia imepelekea kuja kwa wawekezaji wakubwa kutoka nje kufika kuwekeza kwenye uzalishaji wa vifaranga kama hii kampuni ya Organia ambao wanalenga kuzalisha vifaranga na kuuza nje ya Tanzania hivyo kuna kila sababu ya kuzuia vifaranga vya nje ili kulinda soko la ndan”
Naye mfugaji wa kuku, Mwajuma Rajabu alibainisha kuwa vifaranga vya nje vimekuwa vinaharibu ufugaji wa kuku nchini kwa kuwa kutokana na kuingizwa kwa njia za panya wafugaji wa kuku ambao wananunua vifaranga hivyo wamekuwa wavifuga na kisha kuuza kuku kwa bei ya chini kwa kuwa wananunua vifaranga vya magendio vinavyouzwa kwa bei ya kawaida.
“Mimi ninaamini kuwa Rais huyu ni Dk Samia ni msikivu na mtenda haki hivyo anasikia na atasaidia kutusikiliza kwa kuhakikisha serikali yake inakabiliana na uingizwaji wa vifaranga kihoela” anasema Mwajuma