Imeelezwa na Mkurungenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini REA Mhandisi Hassan Saidy kuwa mtu anayetumia nishati ya mkaa na kuni kupikia kwa siku moja nisawa na mtu anayevuta sigara 300 hivyo ni hatari kwa afya na usalama wa mazingira.
Ameyasema hayo katika eneo la Ifakara wilaya ya kilombero Mkoa wa Morogoro wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa kupoza umeme wa Ifakara unojengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya.
“Watu wengi hasa maeneo ya vijijini wanatia nishati ya kuni na mkaa kwaajili ya kupikia na kubwa zaidi kwa vijijini ni kuni ile ya mafiga matatu na unavuta moshi wa kutosha sana na niliambia mtu anayepika kwa kuni na mkaa kwa siku moja ni sawasawa na mtu aliyevuta sigara 300 sasa ubaweza kuona athari yake ni kiasi gani”- Mhandisi Hassan Saidy