Kesi namba 12 ya mwaka 2022 inayowakabili washtakiwa watano akiwemo Makoye Lusana, Masunga Mange Pascal Mange Hoka Mazuri ambae ni mke wa marehemu pamoja na Shija Salum wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kwimba na kusomewa mashtaka yao na mwendesha mashtaka wa Serikali Robert Mwanakatwe huku wakitakiwa kutojibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza keai hiyo.
Inadaiwa watu hao December 1 2022 walimuua Mange Washa kwa madai kuwa alimfukuza mtoto wake nyumbani ambae alikuwa anatuhumiwa kuiba mifugo.
Ndipo Mshtakiwa namba nne aitwaye Hoka Mazuri ambae ni Mke wa marehemu aliwaambia watoto wake wawili ambao nao ni washtakiwa wawatafute watu wengine ili wamuue Baba yao baada ya kuwapata na kuwapa kiasi cha tsh. 800,000 wakatekeleza mauaji hayo ambapo December 5, walitiwa mbaroni na December 14, 2022 wamefikishwa mahakamani na kusomewa shtaka la mauaji linalowakabili.
Hakimu Mafawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Kwimba Ndeko Dustan akaiahirisha kesi hiyo hadi December 28, 2022 itakapotajwa tena kutokana na upelelezi kutokamilika.