Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba amepokea madarasa 29 yenye thamani ya milioni 580 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro ikiwa ni utekelezaji wa agizo lake la kuwataka wakuu wa wilaya kukabidhi vyumba vipya vya madarasa leo tarehe 15/12/2022.
Akizungumza wakati wa makabishiano hayo Mkuu wa Mkoa wa Singida amesema wilaya ya Ikungi imekuwa ya kwanza kwa vipindi viwili mfululizo kumaliza miradi ya ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa kwa mkoa wa singida ambapo amempongeza Dc wa Ikungi Jerry Muro pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya ikungi Justice kijazi na mwenyekiti wa halmashauri Ali mwanga kwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa madarasa hayo ambayo yamekuwa na kiwango bora kinachoendana na thamani halisi ya fedha.
Akikabidhi madarasa hayo katika hafla iliyofanyika katika shule ya Secondary ya isuna mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Muro amemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia wilaya ya Ikungi kupewa milioni 580 na kusisitiza kukamilika kwa madarasa hayo kunatoa fursa ya kuanza maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza mapema mwezi January mwaka 2023 na kusisitiza katika wilaya ya ikungi hakuna mwanafunzi atakaepangiwa katika shule za ikungi atakosa darasa na kiti na meza mana wameshakamilisha pia uwekaji wa viti 1,160 pamoja na meza zake umekamilika kwa shule zote 16 na kilichopo ni wazazi kuandaa watoto.
Wakiongea kwa niaba ya wananchi Mbunge wa jimbo la singida mashariki Miraji Mtaturu pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya ikungi wamewataka wananchi kujiandaa kutumia miundombinu hiyo vizuri kwa kupeleka watoto shule pamoja na kulinda na kutunza miundombinu hiyo uku wakiendelea kumuomba Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuleta fedha zingine za miradi kutokana na miradi kusimamiwa vizuri Ikungi.