Amesema ni lazima Watumishi wa umma wajue wajibu mkubwa ni kuwatumikia Wananchi na kuhakikisha wanatatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye maeneo yao.
Amesema hayo leo wakati wa kikao cha pamoja na Watumishi wa umma wa Halmashauri za Mkoa wa Rukwa ambako alikuwa kwenye ziara ya kikazi.
Amesema Rais Dkt. Samia anataka kuona kila Mtumishi wa umma anawajibika katika kuwatumikia Watanzania “Hawa wananchi wamesambaa katika Wilaya na Halmashauri, tumejenga majengo ya ofisi sio lazima Wananchi waje humo kupata huduma, wapo wengine hawawezi kuja hapa lakini wanahitaji Serikali yao iwahudumie”
Amewataka Viongozi katika kuhakikisha wanasimamia Watumishi kutokaa ofisini wiki nzima badala yake waende vijijini kwani huko ndiko Wananchi walipo ili wawasikilize na kuwatumikia.