Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha, Godwell Ole Meing’ataki akitoa maelezo ya kina kuhusu ikolojia ya hifadhi ya taifa ya Rauha, wakati wa kongamano la wanahabari na wadau wa uhifadhi mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji.
“Mto Ruaha ulikuwa unataririsha maji mwaka mzima hapo zamani, lakini kuanzia miaka ya 90’s ukaanza kuonesha dalila ya kukauka” Godwell Ole Meing’ataki, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha
“Uhai wa taifa unategemea uwepo wa Mto Ruaha” Godwell Ole Meing’ataki, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha
“Ihefu ni chanzo cha Mto Ruaha Mkuu, miaka ya 90 hadi sasa ukubwa wa eneo la Ihefu linasinyaa na kushindwa kukusanya maji kwa ajili ya Mto Ruaha Mkuu, na namna linavyozidi kusinyaa Mto Ruaha Mkuu unaathiriwa” Godwell Ole Meing’ataki, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi
“Mwaka 1985 kulikuwa na hekta 14,000 za kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Ihefu, mwaka 1998 hekta za kilimo cha umwagiliaji zilifika 24,000, mwaka 2013 zilifika hekta 115,000, maji yanaelekezwa zaidi katika mashamba” Godwell Ole Meing’ataki, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi
“Tunavyozungumza Ruaha umekauka ni zaidi ya siku 130 mto hautoi maji japo kuna mvua ndogo imepita” Meing’ataki