Mbali na Sultan wengine ni Kambi Zubery Seif ambaye ni Mmiliki wa Kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Said Matwiko Mkazi wa Magole, Maulid Mzungu maarufu Mbonde (54) Mkazi wa Kisemvule akiwa ni Ndugu na Mtuhumiwa Muharami, John John maarufu Chipanda (40) Mkazi wa Kitunda ambaye jukumu lake lilikua ni kutafuta Vijana wenye vipaji na kuwapeleka Cambiasso Sports Academy pamoja na Sarah Joseph.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine ambazo uzito wake ni kilogramu 34.89 ambapo Wakili wa Serikali Caroline Matemu leo ameieleza Mahakama kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelezi bado haujakamilika hivyo Hakimu Mkazi Mkuu Mery Mrio akaahirisha shauri hilo hadi Januari 2, 2023 kwa ajili ya kutajwa.
Inadaiwa kuwa October 27 2022 eneo la Kivule jijini Dar es Salaam Washtakiwa wote kwa pamoja walisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilogramu 27.10 ambapo katika shitaka la pili inadaiwa Novemba 4, 2022 maeneo ya Kamegele Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Washtakiwa hao kwa pamoja walisafirisha pia dawa za kulevya aina ya heroin.