Ni Desemba 22, 2022 ambapo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Viongozi mbalimbali wamefika katika hafla ya tukio kujaza maji katika bwawa la Julius Nyerere lililopo Rufiji, Mkoani Pwani.
Miongoni mwa Viongozi waliopewa nafasi ya kuzungumza ni Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson.
“Zinapotajwa asilimia za mradi huu (JNHPP) kwamba umefikia asilimia 78.68 ile asilimia ni wastani, ndani ya mradi kuna maeneo yamefikia asilimia 97, 87, 80+. Sasa ukichukua maeneo yote kwa wastani ndio unapata asilimia 78.68”- Spika wa Bunge la Jamhuri la Tanzania Dr Tulia Ackson
Kwa wingi wa maji ya #BwawaLetuLaNyerere tutakuwa na uhakika wa kupata chakula cha kulilisha Taifa na hata dunia” Dkt. Tulia Ackson
Leo inatengenezwa historia ya kuondoa tatizo la umeme nchini, kwa kupata suluhu ya kudumu, Mhe. Rais unafanya, umefanya na kuzidi “- Spika wa Bunge la Jamhuri la Tanzania Dr Tulia Ackson
#BwawaLetuLaNyerere
#HatuaKubwaYaKihistoria #KuelekeaUmemeWaUhakika
Unaweza ukatazama hapa live ushuhudie kile kinachojiri katika tukio hilo la kujaza maji kwenye Bwawa la Nyerere.