Ni Disemba 22, 2022 ambapo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anazungumza katika tukio la kujaza maji kwenye bwawa la Julius Nyerere lililopo Rufiji Mkoani Pwani.
Leo ni siku nyingine ya kihistoria na faraja katika kuelekea safari ya kukamilisha mradi wetu wa Julius Nyerere hatua kwa hatua”- Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye tukio la kujaza maji bwawa la Julius Nyerere
“Nchi yetu chini ya uongozi wa mpendwa wetu Dkt John Pombe Magufuli katika awamu ya tano, tukasema liwalo na liwe lakini azma hii ya Mwalimu (Nyerere) lazima tuitekeleze, mradi huu (JNHPP) utatuletea umeme wa uhakika na endelevu, hatuna budi kuwa shukuru wote waliozaa fikra ya kutekeleza mradi huu”- Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye tukio la kujaza maji bwawa la Julius Nyerere
“MRADI huu (JNHPP) nimepokea ukiwa umefikia 37% na leo najisikia faraja mradi huu kufikia 78.68%. Nitoe ahadi kwenu Watanzania nitausimamia mradi huu hadi ukamilike kama ilivokusudiwa ulivyopangwa.”- Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye tukio la kujaza maji bwawa la Julius Nyerere
“Mradi huu utaimarisha na kufungua fursa nyingi za utalii katika eneo la kusini mwa Tanzania hususan katika hifadhi ya taifa ya Nyerere na hivyo kutoa ajira na moja kwa moja na nyinginezo”- Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye tukio la kujaza maji bwawa la Julius Nyerere