Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameiagiza bodi ya maji ya Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira (tanga-uwasa) kufanya kikao maalum kitakacho washirikisha Wenyeviti wa Serikali za Mitaa,watendaji na Madiwani ili kuweza kubaini changamoto zinazopelekea huduma ya maji kuzorota Jijini hapa.
Kauli hiyo ameitoa katika kikao maalumu kilichohudhuriwa na Maofisa wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira(tanga-uwasa) madiwani na viongozi wa chama cha mapinduzi baada ya ziara ya Waziri huyo kukagua vyanzo hivyo vya maji.
Waziri huyo alisema ipo haja kwa bodi ya maji kuipitia Mamlaka hiyo na kubaini ubadhirifu unaofanywa ili hatua kali zichukuliwe kwa kila mtumishi atakaebainika anakwamisha utolewaji wa huduma bora ya maji kwa wananchi.
“Labda niwaeleze ukweli kipo kitu hapa na katika hiko kikao cha bodi ya maji nami nitatuma watu wangu na hamta wajua ila nikabaini sitiwavumilia nitachukua hatua kali”alisema Waziri Aweso.
“Tanga-Uwasa jipangeni na kila mmoja wenu awajibike lakini kama hamuwezi kujipanga nitakuja kuwapanga kwa nguvu kama mamlaka inavyoniruhusu kwa mujibu wa sheria”Alisema Mh;Waziri.
Mkurugenzi wa Bonde la mto Pangani Segure Segure ikiri kutokea kwa changamoto za uchafuzi wa vyanzo vya maji katima eneo la mto zigi jambo na kuahidi kupokea maelekezo ya Waziri mwenye dhamana ili kudhibiti uharibifu huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanga-Uwasa Geofrey Hill alisema uchafuzi wa maji uliofanyika kwa ghafla ulipelekea mamlaka hiyo kufunga maji ili kuanza kuyatibu kabla hayajaletq madhara kwa wananchi.
“Labda niombe radhi kwa kutokutoa taarifa kwa Wananchi lakini tulichokifanya baada ya maji kuchafuka kwa kiwango kikubwa tuliamua kuyazuia maji kwenda kwa wananchi ili tuyatibu na kuzuia madhara ambayo labda wananchi wangeyapata“Alisema Hily.