Mamlaka ya Afrika Kusini iko katika msako wa Tiger anayemilikiwa na mtu binafsi ambaye alitoroka kutoka Walkerville kusini mwa Johannesburg.
Tiger huyo wa kike alitoroka baada ya uzio kukatwa Jumamosi usiku, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.
Inasemekana kuwa alimshambulia mtu. Pia alimuua mbwa na kumjeruhi mwingine.
Mamlaka ya kuhifadhi wanyama imewataka watu kutomkaribia Tiger huyo aliyepotea kwa usalama wao wenyewe, kwani ni hatari.