Mwili wa mwanamke mmoja Sabina Barma mkazi wa kata ya Ufana wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara umekutwa ukiwa kitandani huku ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.
Ayo TV imezungumza na mashuhuda wa tukio hilo baada ya kufika nyumbani kushuhudia mwili huo.
“Nikifika hapa nikawakuta watoto wakasema mama yao yupo ndani amelala niliita bila mafanikio ndipo nikaenda kufunua bazia nikakuta hali isiyoyakawaida ndipo nikaenda kutoa taarifa kwa wazee”
Mwenyekiti wa kitongoji cha Gisigisi Kijiji Cha Saydoda kata ya Ufana amesema kuwa mwanamke huyo katika shingo yake inaonesha kuwa alichomwa kwa kitu chenye ncha kali.