Mtoto wa kiume wa rais wa Equatorial Guinea amewekwa mbaroni kwa tuhuma za kuuza ndege ya shirika la ndege la taifa hilo kinyume na sheria.
Vyombo vya habari vya serikali vilisema Ruslan Obiang Nsue anadaiwa kuuza turboprop yenye viti 74 kwa kampuni iliyoko Visiwa vya Canary.
Uchunguzi ulianza mwaka jana ilipogundulika kuwa ndege hiyo ilitoweka ilipokuwa ikifanyiwa matengenezo ya kawaida nchini Uhispania.
Mshukiwa huyo alikuwa akiendesha shirika la ndege la Equatorial Guinea, nchi ambayo iko mikononi mwa familia ya Rais Obiang Nguema ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 43.