Makamu wa Rais wa Gambia Badara Alieu Joof amefariki dunia nchini India, kwa mujibu wa tangazo la rais.
Makamu huyo wa rais amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi, ingawa rais hakutaja iwapo alikuwa akipokea matibabu nchini India au la.
Rais Adama Barrow alimteua Bw Joof kama makamu wa rais baada ya kushinda uchaguzi wa marudio mnamo Disemba 2021.
Makamu wa rais aliwahi kuwa waziri wa elimu zamani.