Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa Akizungumza kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kuhusu masuala ya Uchumi amesema hali ya mfumuko wa bei bado ni himilivu na wananchi wanaweza kumudu kufanya manunuzi ya mahitaji muhimu ya kijamii.
Amesema mfumuko wa bei ambao ni tarakimu moja kwa Uchumi hauna madhara makubwa ukilinganisha na mfumuko wa bei wenye tarakimu zaidi ya moja.
Ameeleza kuwa, mfumuko wa bei wa vyakula uliongezeka kasi ya upandaji wa bei kutokana na msimu wa ulizalishaji uliopita kuwa na uzalishaji mdogo wa vyakula kutokana na mvua ambazo zilinyesha kwa kuchelewa katika baadhi ya maeneo.
Amesema Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Desemba, 2022 ulikuwa asilimia 4.8 ukilinganisha na mwezi Novemba, 2022 ambapo Mfumuko wa Bei ulikuwa ni asilimia 4.9.