Wabunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoa wa Morogoro wameoneshwa kutoridhishwa na Kasi ya mkandarasi wa kampuni ya HNXJDL inayotekeleza mradi wa umeme Vijijini (REA) Mkoani Morogoro baada ya kutekeleza asilimia 36 Hadi sasa huku mkataba ukifikia takati mwezi February mwaka Huu.
Akizungumza kwa niaba ya wabunge wa Mkoa huo Mbunge wa Jimbo la Mikumi ambaye ni katibu wa wabunge mkoa Morogoro Mheshimiwa Denis Londo amesema mkandarasi anayetekeleza mradi huo kwenye Wilaya za Kilosa,Kilombero,Ulanga,Malinyi,Mvomero na Gairo ameshafikisha umeme kwenye Vijiji 36 Kati ya vijiji 146 ambayo ametakiwa kufikisha huhuma hiyo hivyo wameoneshwa kutoridhishwa na mkandarasi huyo.
Mheshimiwa Londo anasema Wananchi wa Morogoro wanahitaji Maendeleo hivyo kuchelewa Kwa huduma hiyo inarudisha nyuma maendeleo hasa uanzishwaji viwanda vidogo vidogo
Anasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anahitaji huduma hiyo iwafikie watu wa Vijijini lakini Mkandarasi huyo anachelewesha huduma.
Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya REA Styeden Rwembagila amesema tayari hatua zinachukulia ikiwemo kumpunguzia ukubwa wa eneo la Kazi na taratibu zingine za kisheria zinaendelea kwa Mkandarasi huyo.
Amesema katika mkoa mzima wa Morogoro kulikua na wakandarasi wawili lakini mkandarasi wapili ambaye ni STEG amekamilisha mradi Kwa asilimia 100 ambaye alipewa upande wa Morogoro vijiji lakin mkandarasi HNXJDL ameshindwa kuendana na Kasi ya serikali.