Hapa ni Zanzibar kijiji cha Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja ambapo unafanyika mradi mkubwa wa uwekezaji wa zao la vanila zaidi ya ekari 65 ambazo serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imempatia mwekezaji wa kilimo cha Vanila Simon Mkondya.
Kutokana na uwekezaji huo mkuu wa mkoa wa kusini Unguja Mheshimiwa Rashid Hadid Rashid amefika kujionea uwekezaji huo nakusema serikali ya Rais wa Zanzibar Dkt Husein Mwinyi imekaribisha wawekezaji hususani wa zao hilo ambapo linatajwa kuuzwa hadi shilingi Milioni moja kwa kilo moja nakuwahakikishia wanachi uwepo wa soko la uhakika.