Katibu Mkuu wa CCM ndugu Daniel Chongolo amezindua kitalu cha Miti na kupanda mti katika ofisi ya Bonde Wami/Ruvu morogoro.
Ushauri huo ameutoa leo Februari 5,2023 wakati akizungumza na Watumishi na Maofisa wa ngazi mbalimbali alipokwenda kuzindua kitalu cha miti kwenye ofisi ya Bonde Wami/Ruvu mkoani Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine ameelezwa vitalu vya miche ya miti hiyo inahifadhi mazingira na kutunza maji.
Aidha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameshauri kuanzishwa kwa vikundi vya uhifadhi mazingira kwenye maeneo mbalimbali ya mito ili kushiriki kikamilifu kutunza mazingira kwa lengo la kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwenye jamii.
Kwa Upande wake mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Elibariki Mmasy akitoa maelezo kwa Katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo amesema Shamba hilo litakuwa kichocheo kikubwa katika Suala zima uhifadhi na utunzaji wa mazingira hasa katika vyanzo mbalimbali vilivyo chini ya Bodi hiyo ya maji.