Usiku wa Jana 11 February, 2023 kumefanyika Tuzo za Ujenzi Afrika Mashariki, ni Tuzo zilizoandaliwa na Kampuni ya Masoko ya Bidhaa na Huduma za ujenzi iitwayo Ujenzi Media Group kw,a kushirikiana na Global Construction International Film.
Tuzo hizi zilikuwa zikiwaniwa na Makampuni Zaidi ya 500 kutoka Afrika Mashariki.
Akizungumza na Wanahabari Steven Mkomwa ambae ni Katibu wa bodi ya Tuzo za Ujenzi za EABC (EAST AFRIKA BUILDINGS AND CONSTRUCTION AWARDS).
Amesema Tuzo hizi ni za Mara ya kwanza ambazo wameziratibu kwa kushirikiana na Washirika wao Global Construction International Film na ni Tuzo za mwaka 2022 ambazo hazikuweza kutolewa mwaka 2022 Desemba kwa sababu za kimaandalizi.
Mkomwa amebainisha kwa kusema Dirisha la kupokea mapendekezo kwaajili ya Tuzo za mwaka 2023 litakuwa wazi tarehe 1 Julai 2023 na Tuzo zake kutolewa 25 Novemba, 2023 ambapo aliongeza kwa kubainisha kuwa Tuzo hizo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa Zaidi kwani Kamouni nyingi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zitashiriki.
Mkomwa alisema Sekretarieti ya Tuzo hizo inatarajiwa kusafiri nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuweza kuongeza uelewa na ushiriki wa chapa na wadau wa sekta ya ujenzi ndani ya Jumuiya.