Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Salum Awadh, amesema kupanda kwa chakula kunatokana na changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji hafifu kwa mbolea kunakochangiwa na hali ya Vita ya Ukrani na Urusi
Ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wadau wa bodi hiyo.
Mbali na jitihada hizo amesema kwa sasa bodi inapanga kununua mazao kwa wingi kutoka kwa wakulima na kuweka ziada ya chakula ambapo amesema bodi hiyo inaweza kununua mazao yenye thamani ya bilioni 50 huku ikitarajia kuongeza kiasi hicho cha fedha na kufikia bilioni 100.
“Sisi tunauwezo wa kununua mazao mpaka bilioni 50, lakini bajeti yetu ya mwaka huu wa fedha unaoanza fedha tumeongeza bajeti mara mbili mpaka bilioni 100”