Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Pilsner Lager imefanya droo ya kwanza ya promosheni yake pendwa ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’ kubainisha Washindi wa kwanza wa promosheni hiyo ambayo ni maalumu kwa wateja wa bia hiyo wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini.
Kupitia promosheni hiyo inayofanyika kwa muda wa wiki 8, wateja wa bia ya Pilsner watajishindia zawadi mbalimbali zikiwemo, televisheni, simu janja, pikipiki na zawadi ya mwisho ya gari. Droo iiliyofanyika jana, walipatikana washindi 7 kutoka kanda zote tatu, ambapo mshindi mmoja kutoka kanda ya Ziwa alishinda pikipiki, wengine watatu kutoka kanda zote tatu walishinda simu janja na wengine watatu walishinda televisheni. Washindi hao wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao tarehe 18 mwezi huu.
Akizungumza wakati wa droo hiyo, Meneja wa bia ya Pilsner, Wankyo Marando alisema, droo hiyo ni mwanzo tu wa promosheni ya ‘Kapu la Wana’, akitoa wito kwa wateja wa bia ya Pilsner mikoa ya kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini kuendelea kushiriki kwenye promosheni hiyo kwani zawadi ni nyingi.
Hii ni mara ya pili bia ya Pilsner imekuja na promosheni hii ya ‘Kapu la Wana’ na imetenga zaidi ya Tsh. 36 milioni kwa Washindi 22 wa kampeni hiyo.