Maafisa wa New Zealand wanasema watu wasiopungua wanne, akiwemo mtoto, wamefariki kutokana na uharibifu wa kimbunga Gabrielle, ambacho kimesababisha mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi katika kisiwa hicho cha Kaskazini.
Helikopta za uokoaji huko zilikuwa zimewaokoa takriban watu 300 waliokuwa wamekwama kwenye mapaa. Kimbunga hicho kimeondoka nchini New Zealand lakini takriban watu 10,500 bado wameyakimbia makazi yao siku ya Jumatano.
Waziri Mkuu Chris Hipkins Jumatano jioni alisema pia kuna “watu kadhaa ambao hawajulikani waliko ambao polisi wanawashikilia wasiwasi mkubwa”.
Wakati huo huo, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.0 lilishuhudiwa kote nchini jumatano jioni. Hakukuwa na ripoti za haraka za uharibifu au majeruhi kutokana na tetemeko hilo, lililotokea pwani ya kisiwa cha Kaskazini karibu na mji mkuu Wellington.