Watanzania 170 wanatarajiwa kupata mafunzo maalumu katika kada mbalimbali ili kushiriki kikamilifu kwenye miradi ya gesi na mafuta inayotekelezwa hapa nchini.
Akizunguza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wanafunzi mia moja na sabini kutoka EACOP katika chuo cha Veta mkoani Tanga Kamishina wa Petroli na Gesi nchini Michale Mjinja amesema kuwa Mradi wa Bomba hili kutoka hoiama nchini Uganda hadi chongoleani nchini Tanzania takribani asilimia 80% ya bomba hilo.
Aidha inaelezwa kuwa mafunzo hayo ni nafasi nzuri ya watanzania kujifunza ili kuweza kupata ujuzi huo,ambapo lengo la mafunzo hayo ni kuwaanda watanzania kupata elimu inayo kizi viwango na sifa za kimataifa katika ujenzi wa miradi ya mafuta na gesi.
“tutambue kwamba mradi huu wa mafuta gafi kutoka ohima nchini Uganda hadi hapa tanzani ni mradi wa kimkakati wa nchini zote mbili unaolenga kuwawezesha wananchi wake na wawekezaji kunufaika kiuchumi katika kuhakikisha hilo serikali inayo ongozwa na jemedari wetu Mhe.Rais Samia Suluhu Hasani imeendelea kuchua hatua mbalimbali za kimsingi za kuwawezesha watanzania hatua hizo ni pamoja na kutenga kazi na huduma katika mradi huu ziweze kutolewa na watanzania pekee”- Alisema Mjinja
Aidha Kamishina wa Petrol na Gesi amesema kuwa sSrikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuwawezesha watanzania kunufaika na mradi huo ambapo hadi sasa Serikali imeendelea kuwajengea uelewa watanzania juu ya kufahamu mradi huo ambapo hadi sasa Makampuni takribani miamoja Arobaini na sita ya kitanzania na watanzani elfu moja na mia sita wanaendelea kushiriki kwenye mradi huo.
Hata hivyo Kamishina Mjinja ametoa msimamo wa Serikali katika mradi huo kuwa mradi utatekelezwa kama kawaida kwani mradi huo unatekelezaji kwani unakidhi Viwango vya kimataifa katika maswala Mbalimbali ya kimazingira,haki za kibinadamu na kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijazo hivyo serikali ina watoa hofu watanzania kuwa mradi huo utatekelezwa kama ulivyopangwa kwa kuzingatia tarati na Sheria za nchini na taratibu za kimataifa.