Licha ya kuwepo Kwa Wadau mbalimbali wa kupinga uharibifu wa mazingira na Rasilimali za maji bado hali ya uchafunzi umekua mkubwa ambapo wanawake wametakiwa kushiriki kikamilifu katika harakati Hizo.
Wakizungumza mjini Morogoro Kwenye semina ya Siku mbili kilichoketi kuanzia February 22 na 23 Mwaka huu iliyoandaliwa na Shahidi wa Maji wanaharakati wa kutetea na kupinga uharibifu wa rasilimali za maji wamesema wanawake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele.
Akitoa mada katika mkutano huo Mmoja wa wanaharakati hao Bi. Gemma Akilimali amesema wanawake ndio waathirika wakubwa wa ukosefu wa Maji hivyo endapo watashirikishwa ipasavyo itasaidia kwani ndio watumiji wakubwa wanatambua umuhimu wake.
Anasema katika mabaraza ya utunzaji maji yanayoundwa kuwe na asilimia hamsini kwa hamsini Kati ya wanaume na wanawake ili kuweka usawa katika mapambano hayo kuwa na nguvu ya pamoja.
Kwa upande wake afisa miradi SHAHIDI WA MAJI Bwana John Emanuel amesema Lengo la semina hiyo ni kutoa Elimu Kwa jamii kuona umuhimu wa utunzaji vyanzo vya maji pamoja na rasilimali zake.
Anasema anatambua jitihada zinazofanywa na serikali katika uthibiti uharibifu wa mazingira lakini taasisi hiyo inaendela kukumbusha jamii umuhimu wa Jambo Hilona athari zake.
Serikali imeendelea kusisitiza jamii kutunza vyanzo vya maji pamoja na rasilimali zake ili kuepukana na changamoto ya uhaba wa Huduma hiyo huku mabadiliko tabia nchi ikiwa ndio Chanzo kikubwa cha matatizo.