Khloe Kardashian amefunguliwa kesi na aliyekuwa msaidizi wake wa nyumbani ambaye anadai alifukuzwa kazi baada ya kuchukua likizo baada ya kuumia mguu.
Matthew Manhard, ambaye alianza kufanya kazi kwa staa huyo mnamo 2019, na anadai aliacha kufanya majukumu yake mnamo Novemba 2022
na anadai kwamba alimwambia Khloe kwamba hakuweza kufanya kazi kutokana na jeraha lake Mei 2022 na anasema aliporejea kazini miezi sita baadaye, alisimamishwa kazi.
Manhard, ambaye anatafuta fidia ya fedha, pia anadai kuwa hakulipwa muda wa ziada katika siku alizofanya kazi kwa zamu ya saa 12, hata hivyo, wawakilishi wa Kardashian wamekashifu na kukataa madai hayo.
Hii si mara ya kwanza kwenye familia ya kardashian kwani hata Kim Kardashian aliwahi kukabiliwa na kesi kama hiyo mnamo 2021 ambapo walalamikaji walidai mama wa watoto wanne alichelewa kulipwa, alizuia asilimia 10 ya mishahara yao kwa ajili ya kodi lakini hakupeleka kiasi hicho kwa serikali na alikataa kuwalipa muda wa ziada, na wakati mwingine kuwalazimisha kufanya kazi bila mapumziko ya kupata chakula.