Denis Wong, 60, alikamatwa Machi 2022 katika msako wa siri katika jumba lake la mafunzo ya karate ambapo polisi walisema yeye na msaidizi wake walikuwa wakifundisha “combat tai chi”.
Polisi walisema walikamata silaha, ikiwa ni pamoja na mapanga, pinde na mishale yenye ncha ya chuma, wakati wa uvamizi nyumbani kwake.
Baadaye Wong alikiri kosa la kuchochea uasi, kosa ambalo linaweza kuadhibiwa hadi miaka 10 jela.
Wong alishutumiwa kwa kuchapisha jumbe za kuipinga serikali kwenye Facebook, zikiwemo wito wa kuangusha serikali ya Hong Kong na China na kuanzisha “serikali kivuli na kikosi cha kujilinda”.
Zaidi ya watu 230 wamekamatwa chini ya sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong na zaidi ya 140 kati yao wamekabiliwa na mashtaka.
Maafisa wa magereza ya jiji hilo walisema wiki hii kuwa hadi mwisho wa mwaka jana, watu 522 walisalia gerezani kuhusiana na maandamano ya 2019 au ukiukaji wa usalama wa kitaifa.