Wakala wa maji vijijini Ruwasa mkoa wa Tanga imesaini mikata nane ya maji kwa Wilaya tano wenye thamani ya bilioni kumi ili kutatua changamoto ya maji mkoani hapa.
Akizungumza mara baada ya kusainiwa mikataba hiyo Mkuu wa mkoa wa Tanga Omary Mgumba amewataka wakandarasi hao kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa uwadilifu mkubwa na kuwatumia Wananchi wa maeneo husika ili kutekeleza miradi hiyo ili kuwawezesha wazawa kunufaika na miradi hiyo kwenye maeneo yao.
“Nampongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassani kwa kutuletea miradi mikubwa ya Maji mkoani Tanga na taifa kwa ujumla hakika tunamshukuru sana hata kwa motambo ya uchimbaji wa visima pamoja na mitambo ya uchimbaji wa mabwawa hakika Mhe.Rais amedhamiria kutatua changamoto ya maji Hapa nchini.”
Aidha RC Mgumba amesema kuwa kusainiwa kwa mikataba hiyo kati ya Serikali na wakandarasi juu ya usambazaji wa maji lengo ni kuwawezesha Wananchi kuwa na maisha bora na kupata maji safi na salama ambapo vijiji vitakavyo nufaika kutoka na mikata hiyo ya maji ni vijiji 20 ambapo Wilaya zitakazo guswa ni wilaya tano kati ya nane za Mkoa wa Tanga.