Meli kubwa ya mzigo kutoka Nchini Urusi yenye urefu wa mita 150 imetia nanga kwa mara ya kwanza kwenye Bandari ya Tanga baada ya kukamilika kwa ujenzi wa gati lenye urefu wa Mita 300.
Akiongea wakati akipokea Meli hiyo iliyobeba shehena ya mbolea kwa ajili ya Viwanda vya madini, Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha amesema kuwa ujio wa Meli hiyo ni matunda ya uwekezaji uliofanywa na Serikali kwenye Bandari ya Tanga.
Amesema Meli hiyo imebeba mzigo wa tani 6909 unaopelekwa kwenye Nchi ya Congo ambapo utapakuliwa kwa muda wa siku mbili kuanzia leo… “niwaambie Wafanyabiashara, Bandari ya Tanga imefunguka kutokana na maboresho hayo na sasa hata huduma zetu zimezidi kuimarika hivyo niwaombe waje kuitumia bandari ya Tanga”