Taarifa iliyosambaa kuhusu kulipuliwa kwa jengo la bunge la Somalia imehusishwa na Kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab ambapo inasemekna kundi hilo limeshambulia bunge la Somalia na kusababisha vifo vya watu kadhaa mjini Mogadishu.
Milipuko na milio ya risasi imesikika huku bunge likiendelea na mikutano yake ndani ambapo Gari lililokuwa na mabomu lilipuka leo kabla ya saa sita mchana na kufuatiwa na milipuko mingine pamoja na milio ya risasi.
Wabunge pamoja na baadhi ya wafanyakazi wengine waliokolewa muda mfupi tu baada ya gari hilo kulipuka,Mashambulizi hayo bado yanaendelea huku wapiganaji hao wakifyatua risasi wakiwa ndani ya msikiti mmoja karibu na majengo ya bunge.
Bunge hilo ambalo huendesha vikao vyake mjini Mogadishu limewahi kushambuliwa ikiwemo mwaka 2009 na 2010,Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti mkubwa wa miji kadhaa nchini Somalia lakini bado linadhibiti maeneo mengi ya vijijini.