Hospitali ya Wilaya ya Ubungo imesema ina uhitaji wa damu kutokana na uwepo wa huduma za uzazi hospitalini hapo na matukio ya ajali za mara kwa mara katika barabara ya Morogoro.
Akizungumza na Ayo Tv, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr.Imani Mwelang’ombe amesema;
“Tunawapongezawatu wa Fire of GOD Ministry kwani Hospitali yetu ni mpya, huduma zikiwa zimeanza na majengo yakiwa yanaendelea, hivyo wametufungulia milango kwani uhitaji ni mkubwa kuna wajawazito, wagonjwa na pia tupo karibu na barabara ya Morogoro,”.
Kwa Upande wake Mchungaji wa Kanisa la Fire of God Ministry, Swide Mlay amesema.”Leo tupo watu 25 ambao tumekuja kuchangia damu, utakuwa utaratibu endelevu kwa kila baada ya miezi mitatu tutakuwa tunatoa damu”
“Kilichotusukuma hasa ni mwezi wa pili tulikuwa kwenye mfungo wa siku 21 sawa na neno la Mungu linavyosema tusijifunge na ndugu wa damu, leo tumekuja kutoa damu ambayo inaweza kusaidia ndugu zetu, jamaa zetu kama sasa hivi matukio ya ajali yamekuwa mengi, hivyo hitaji la damu limekuwa kubwa,”.amesema.