Katika shauri hilo namba 217 la mwaka 2022 mpeleka maombi ambaye ni Kishoa kupitia Wakili wake Eden Kilatu ameiomba Mahakama ione ndoa yake na David Kafulila imevunjika kiasi cha kutorekebisha, hivyo ivunjwe kwani walitengana tangu mwaka 2019.
Katika hukumu hiyo ambayo imetolewa na Hakimu Mwandamizi Swai S.O ameeleza kuwa hana mashaka kuwa ndoa hiyo imevunjika kiasi cha kutorekebishika chini ya kifungu 107 (2) (f) cha sheria ya ndoa.
“Kwa msingi huo amri ya kuivunja ndoa na talaka inatolewa.
Sambamba na hilo, Watoto wataishi chini ya uangalizi wa Mama yao, Kafulila atakuwa na haki ya kuwaona na kuwa na Watoto wake mwishoni mwa juma na vipindi vya likizo za masomo”
Pia kupitia nakala ya hukumu hiyo imeeleza kuwa chini ya kifungu 129 cha Sheria ya Ndoa, mjibu maombi anawajibika kutoa matunzo ya Watoto kikamilifu ikiwe ada za Shule ambazo zilipwe kwa uwiano linganifu (asilimia 50) kwa kila Mzazi katika Shule watakazokubaliana pamoja.
Ndoa hiyo iliyofungwa Aprili 22, 2014 ilivunjwa rasmi Februari 20, 2023 baada ya Wanandoa hao kutengana tangu mwaka 2019.