Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameagiza kukamatwa na kuhojiwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Club ya Yanga Dkt.Mshindo Msola ambaye ni Meneja mauzo wa kampuni ya mbolea ya minjingu kutokana na ghala la mbolea hizo la Mkoa wa Njombe kukamatwa na mifuko 776 iliyojazwa mchanga badala ya mbolea kwa ajili ya kwenda kuwauzia Wakulima.
Bashe amenukuliwa akisema “Huyo mtu wa TFRA aliyekuja hapo akachukua sampo mchukueni wekeni ndani atoe maelezo, Watu wa minjingu wachukueni wawekeni ndani watoe maelezo na ufanyike uchunguzi wa kutosha na mimi nitatoe statement, mpelekeni Polisi hadi Msola akatoe maelezo”
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ametoa pole kwa Wananchi kutokana na adha ambazo wanakutana nazo huku akiagiza Wafanyabiashara wa mbolea kuzingatia uaminifu, uzaleno na utaifa.