Mbunge Viti maalum mkoa Mwanza Furaha Matondo amepeleka tabasamu kwa watu wenye mahitaji maalum (Walemavu) kwa kuwapatia Wheelchair 70, pamoja na fimbo maalum 30 kwa watu wasioona.
Mbunge huyo ameeleza namna alivyowahi kuguswa na Watu wenye ulemavu na kuahidi kuendelea kuwashika mkono wenye uhitaji kwa kuwapunguzia changamoto walizonazo.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima ameitaka jamii kulitazama kundi la wenye ulemavu kwani wengi wao wanapitia changamoto ambazo sio rahisi kuzisema kwa mtu mmoja mmoja na kuongeza kundi hilo linamchango mkubwa kwenye Taifa.