Club ya Yanga imesema iko tayari kumruhusu Mchezaji wake Feisal Salum kuondoka kwa kuzingatia matakwa ya mkataba na utaratibu wa sheria za uhamisho wa Wachezaji zinazotambulika na TFF pamoja na FIFA.
Taarifa rasmi ya Club hiyo iliyotolewa jioni ya leo pamoja na kumtaka Mchezaji huyo kuripoti kambini imetoa wito huo kwa Club inayomtaka.. “Ikiwa pia kuna Timu yoyote inahitaji huduma ya Mchezaji huyu, Yanga iko tayari kufanya mazungumzo wakati wowote”