Mawakili wa CHADEMA wameondoa nia ya kuwahoji maswali ya dodoso Halima Mdee, Ester Bulaya na Ester Matiko juu ya kiapo kinzani walichowasilisha katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam katika kesi waliyofungua kupinga kuvuliwa uanachama wa Chama hicho.
Mbali ya hao, wabunge wengine katika shauri hilo ni Halima Mdee, Grace Tendega, Nursat Hanje, Cecilia Pareso, Hawa Mwaifunga, Esther Matiko, Esther Bulaya, Jesca Kishoa, Felister Njau, Agnesta lambart, Asia Mohamed, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Styella Siyao, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza na Naghenjwa Kaboyoka.
Hatua hiyo imefikiwa leo mbele ya Jaji Cyprian Mkeha baada ya wakili wa CHADEMA, Hekima Mwasipo kuieleza Mahakama hiyo kuwa wameamua kufunga maswali hayo baada ya kutafakari kwa kina na kubaini kwamba hawana maswali ya ziada kwa Wabunge hao.
Shauri hilo namba 36/2022 leo liliitwa Mahakamani hapo kwa ajali ya Mbunge Jesca Kishoa kumalizia kuulizwa maswali ya dodoso na mawakili wa Chadema kuhusu malalamiko yake ya kufukuzwa uanachama kinyume cha Sheria, lakini wakili Mwasipo akadai kuwa wamefunga kumuuliza maswali hayo.
Baada ya kuwasilisha ombi Hilo, Jaji Mkeha alikubali ombi la kufunga maswali ya dodoso, kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 9,2023 ambapo wajumbe watakaoanza kuhojiwa ni Dk. Lwaitama na Ruth Molel baada ya Mdee na wenzako kutaka Wajumbe hao wa Bodi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA nao wahojiwe.