Wakuu wa sekta ya afya barani Afrika wamekutana mjini Kigali, Rwanda, kujadili njia za kujenga upanuzi wa mifumo ya afya ili kujibu matishio yanayoibuka na yaliyopo kama athari za mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza katika Mkutano wa 5 wa Kimataifa wa Ajenda ya Afya ya Afrika (AHAIC) kwa mwaka 2023, Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) Ahmed Ogwell Ouma ametoa wito kwa uwekezaji zaidi katika kujenga namna rahisi kwenye mifumo ya afya katika bara la Afrika.
Amesema mifumo ya pande nyingi mara nyingi haijatimiza mahitaji ya bara hilo, na janga la COVID-19 limetumika kama ukumbusho wa ngazi ya Afrika ndani ya mfumo wa ngazi ya afya duniani.
Ameongeza kuwa, mabadiliko ya tabianchi yako katikati ya majanga na dharura za afya zinazoshuhudiwa sasa, na zinasababisha mambo mbalimbali, ikiwemo hasara za kiuchumi.
Mkutano huo unaofanyika kila baada ya miaka miwili utatoa jukwaa kwa Afrika kuleta mazingatio ya kimataifa kwa uhusiano usiopingika kati ya mabadiliko ya hali ya hewa na afya wakati dunia inapokaribia makataa ya Malengo ya Kidunia ya 2030.