Wasichana 28 Wamelazwa Hospitalini Kwa ‘Wasiwasi’ Baada ya Kucheza na “Ouja bord”Shuleni Nchini Colombia
Kwenye historia bodi za Ouija ziliundwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani mwaka wa 1886. Tangu wakati huo zimekuwa maarufu katika hadithi za uchawi, hasa kutokana na madai ya uwezo wa washiriki wake kuwasiliana na marehemu.
Wanafunzi hao walipewa rufaa kwenye hospitali ya manispaa ya eneo hilo kulingana na itifaki zilizowekwa.
Wakurugenzi na walimu waliandamana na wanafunzi wakati wa mchakato wa tathmini huku Wazazi na walezi husika walijulishwa hali wakati huo.
Akitoa taarifa kuhusu tukio hilo la kutisha la shule, Hugo Torres, ambaye ndiye mkuu wa shule yenye makao yake makuu Colombia, alisema, “Kulikuwa na visa 28 vinavyowezekana vya wasiwasi kwa wanafunzi wa shule na kwa kuzingatia maoni yalitolewa kwa jamii ambayo, badala ya kusaidia kutatua hali hiyo, ilisababisha mkanganyiko na mazingira mabaya kwa kazi yetu. Walidai ni uchawi!
Torres alihitimisha, “Shule inasubiri uchunguzi wa kimatibabu ili kutoa habari zaidi ya kuaminika huku taasisi ya elimu pia ikiwaomba kwa heshima wananchi wajiepushe kufanya maamuzi ya mapema na uchunguzi wao wenyewe.
“OUIJA BOARD” inajulikana kama “board spirit”au “talking board” ni ubao bapa ulio na herufi za alfabeti ya Kilatini, nambari 0-9, maneno “ndiyo”, “hapana”, mara kwa mara “hello” na “Goodbye”, pamoja na alama mbalimbali na graphics.
Inatumia planchette (kipande kidogo cha mbao au plastiki yenye umbo la moyo) kama kiashirio kinachohamishika ili kutamka ujumbe wakati wa wakucheza.
Washiriki huweka vidole vyao kwenye planchette, na inasogezwa karibu na ubao ili kutamka maneno. yaliyo semekana ya kichwawi kuwaita waliokufa.