Leo Machi 08,2023 siku ya wanawake dunia mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka wanawake mkoani hapo kuacha kuwaagiza Watoto porini kutafuta kuni kwani huko matukio mengi ya Ulawiti na Ubakaji hutokea.
RC Senyamule ameelekeza hayo wakati akikabidhi misaada ya mitungi ya gesi na majiko banifu yanayotumia kuni na mkaa mchache ili kupunguza athari za Uharibifu wa mazingira katika vijiji vya Zanka na Kigwe msaada uliotolewa na Jumuiya ya wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Senyamule amesema tofauti na ukatili ambao wanayapata watoto kutoka kwa watu wazima,Wanawake wamekuwa wakipata athari nyingi kwa kutumia kuni mojawapo ni magonjwa ya kiafya kwa maana ya macho na kifua hivyo kujikuta wakishindwa kuendelea na uzalishaji na badala yake kaunza kujitibu.
“Hivi karibuni kumazuka matukio ya ukatili wa Watoto nawaomba msiwaruhusu watoto waende peke yao kutafuta kuni maporini huko wanaweza kufanyiwa ukatili wa kubakwa na kulawitiwa”–RC Dodoma
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Teknolojia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage, amesema wameamua kuwasaidia wakazi wa Vijiji vya Zanka na Kigwe kutokana na umaskini uliopo katika maeneo hayo.
“REA tumekuja kuhamashisha jamii tunaenda kuwekeza nguvu katika nishati ya kupikia ni kama hizi mmeona majiko ambayo yanatumia mkaa kidogo unapika vyakula vingi”–.Eng. Mwijage
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gondwe amesema atashirikiana na viongozi wa vijiji na kulinda mazingira.