Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda akiwa Dodoma leo amesema “Vijana hawa walifanya mafunzo JKT na walipotimiza miaka miwili wakapewa vyeti baada ya kukosa fursa aidha kuandikishwa JWTZ au katika Taasisi/Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, walirejeshwa majumbani lakini sasa fursa imepatikana, naishukuru Serikali tumepata nafasi kuandikisha Vijana hawa”
“Kijana anatakiwa awe Raia wa Tanzania wa kuzaliwa umri wa miaka 18-26 kwa Form IV hadi Form VI, kwa wenye elimu ya juu kufikia shahada ya uzamili umri usizidi miaka 27, awe na afya nzuri ya mwili na akili, tabia njema, nidhamu nzuri na awe hajawahi kupatikana na kosa la kijinai au kushtakiwa Mahakamani na kufungwa, vilevile awe na cheti halisi cha kuzaliwa, vyeti vya Shule na taaluma na pia awe hajawahi kutumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo na Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo na awe na cheti cha kuhudumia JKT kwa miaka miwili”
“Maombi kwa mkono yawasilishwe Makao Makuu ya Jeshi Dodoma kuanzia hivi sasa ninavyotangaza hadi March 20,2023, yatumwe kwa Mkuu wa Utumishi Makao Makuu ya JWTZ, P.O.BOD 194 Dodoma, Tanzania au pia kupitia ulinzimagazine@tpdf.mil.tz”