Akiwa madarakani tangu 2013 na kuchaguliwa kama rais kwa mara ya kwanza mwaka 2018, Xi Jinping alichaguliwa tena kwa kauli moja, bila ya kushangaza, kuwa rais wa China Ijumaa Machi 10, katika kura ya wabunge.
Ataongoza China kwa muhula wa tatu wa miaka mitano, jambo ambalo halijawahi kutokea nchini humo.
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 69 tayari alikuwa amepata nyongeza ya miaka mitano Oktoba 2022 kuwa mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha CCP na mwenyekiti wa tume ya kijeshi, nyadhifa mbili muhimu zaidi za madaraka nchini humo.
Kuchaguliwa kwake tena ni kilele cha ongezeko ambalo limemfanya kuwa kiongozi mwenye nguvu zaidi nchini tangu vizazi kadhaa.
Xi Jinping yuko madarakani kwa miaka kumi, na hapa anatarajia tena kuongoza China kwa miaka mingine mitano. Hakukuwa na mashaka yoyote juu yake.
Xi Jinping amechaguliwa tena Ijumaa Machi 10 kuwa rais wa China kwa muhula wa tatu, jambo ambalo halijawahi kutokea nchini China, baada ya kura rasmi.