Wachimbaji wadogo wa madini mkoani Katavi wamepata Shilingi 262 ndani ya miezi miwili baada ya kuuza Marudio ya kutoka Migodini “Makinikia” huku ikielezwa mtu mmoja anapata hadi Sh. Milioni 20.
Hayo yamebainishwa wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko baada ya kuutembelea mgodi wa Uchimbaji Madini Katavi Mining ambao unatumia teknolojia ya Kisasa kuchenjua “Makinikia” wanayoyachukua kutoka kwa wachimbaji wadogo.
“Tumepata soko la kuuza Makinikia yetu, hivyo tunaiomba Serikali iendelee kuulinda mgodi huu kwani kwa muda wa miezi miwili tumeuza Tani 15,000 yenye thamani ya Shilingi Milioni 262 siku 40”
“Mwanzo tulikuwa tunalundika tu malundo ya mlima kulikuwa hakuna pa kuyapeleka ambapo labda mtu akiamua anakwenda kuyaosha na anapata Shilingi Elfu Tano ama Elfu Kumi kifupi yalikuwa hayana thamani,” William Mbogo – Mmiliki wa Migodi na Mwakilishi wa Wachimbaji Wadogo Katavi.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa, Mrindiko amesema…”Kiwanda hiki cha Katavi Mining ndani ya mkoa wa Katavi kwa sada hivi hatuna mgodi mkubwa kama huu, huu ndio mgodi namba moja kwa ukubwa kwa sasa hivi kwa maana hiyo ni mgodi muhimu sana kwa uchumi wa mkoa wa Katavi lakini pia kwa mapato ya Serikali kwa maana ya Serikali, nasema hivyo kwa sababu hadi sasa hivi nikiorodhesha walipa kodi wa TRA anayelipa kodi nyingi serikalini kupitia TRA ni Katavi Mining lakini anayetoa mapato makubwa kwenye sekta ya madini ni Katavi Mining,
“Pamoja na hayo kuna ajira ya watu takribani 522 wale ambao wapo permanent na wale ambao machimbo yao ama material wanayochimba maeneo mengine wanakuja kuyauza hapa,”.
Naye Meneja Mwajiri wa Katavi Mining Twalib Seif amesema; “Mpaka sasa kampuni yetu imeweza kusafirisha Kontena 202 tangu tulipoanza kazi zetu Machi 21,2022 hivyo Kampuni yetu inashirikiana na wachimbaji wadogo wadogo kwa kununua malighafi ambayo tunaileta hapa na kuizalisha ambapo inawaongezea kipato, kwani malighafi tunayonunua ni marudio ambayo wao walikuwa hawawezi kuyafanyia kazi ila kupitia mtambo wetu tunaweza kuchenjua na kuongeza thamani,”.