Leo Machi 10,2023 Waziri wa Madini Dkt. Dotto Biteko amemtaka katibu mkuu mpya wa wizara hiyo kuhakikisha kila mfanyakazi wa wizara hiyo anafanya kwazi kwa kujituma ili iwe kivutio kwa kila mtu kutamani kufanyakazi katika wizara hiyo
Hayo ameyasema hayo jijini Dodoma kwenye kikao chake na watendaji wa Wizara na Taasisi zilizochini ya wizara wakati akimkaribisha na kumtambulisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Kheri Mahimbali.
Dkt.Biteko amesema katika wizara hiyo wapo watu wa kada mbalimbali wanaoweza kukwamisha na wengine wanamalengo mema ya kuhakikisha wizara hiyo inapiga hatua hivyo anapaswa kuwa makini ili kuhakikisha kazi zinafanyika na kufikia malengo ya serikali kama ambavyo yamepangwa.
“Wapo watu wa kila aina wapo ambao ukiwapa kazi wao wanaangalia ‘dead line’ hata kama kazi uliwapa haijakamilika wanakuletea, lakini wapo ambao kazi hawamalizi kwa wakati na wala majibu hawakupi lakini pia wapo ambao wao kazi hawafanyi kabisa, lakini wapo wengine ambao wao ukiwapa kazi wanafanya na ukiwarekebisha wanafurahi kurekebishwa lakini wengine ukiwarekebisha wanakukasilikia”.…Waziri wa Madini Dkt. dotto Biteko
Kheri Mahimbali katibu Mkmkuu wa Wizara ya Madini amewataka wataalam wa Wizara kuweka msukumo kwenye madini ya Kimkakati kutokana na umuhimu wa madini hayo katika kuyafungamanisha na sekta nyingine za kiuchumi.
‘’Tumeletwa hapa kuongeza nguvu, sikuja kumwondoa yoyote kwenye nafasi yake, bado tuna kazi mbele yetu na ninaamini katika kushirikiana tutafika mmbalimbali katika kuyatimiza malengo ya Sekta ya Madini’’. Mahimbali Katibu Mkuu Wizard ya Madini.