Huku Tanzania ikiwa inaadhimisha miaka miwili ya Uongozi wa Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan baadhi ya mataifa Duniani ikiwemo Canada Shelisheli pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika wamesema katika miaka hiyo miwili Uongozi wa Rais Samia umeweza kukuza Diplomasia na hivyo kuimarisha mahusiano na mataifa mengi na kuimarisha uchumi wake.
Baadhi ya mabalozi wa Nchi hizo akiwemo Balozi wa Sheli sheli Nchini Maryyoune Pool .Charlote Assack Masias Balozi wa Nchi ya Sweeden Nchini pamoja na Patricia Laverley ambao wameshiriki mkutano wa wanadiplomasia Wanawake uliofanyika jijini Dar es Salaam leo wamesema ndani ya miaka miwili ya uongozi wa Rais Dokta Samia ameweza kuimarisha Diplomasia na mataifa ya Nje hali iliolifanya Taifa la Tanzania kufanya vyema katika masuala mbalimbali kama Uchumi na Miradi ya Maendeleo.
Kwa upande wake mwana diplomasia na Waziri Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Sita Balozi Liberata Mulamula amesema ndani ya miaka miwili ya Rais Dkt Samia ameonesha umahiri kwa kufungua mahusiano na Mataifa mengi hali ilioimarisha diplomasia ya Taifa la Tanzania .
Naye Kanel Mmoshi mwanzilishi wa Taasisi ya diplomasia amesema kitendo cha Rais Samia kufungua Nchi na kuimarisha Diplomasia kumepelekea maendeleo makubwa ikiwemo ya kimiundombinu huku akiahidi kuendelea kuzalisha wana diplomasia wengi ili kumsaidia Rais Samia katika kukuza maendeleo ya Nchi.
Rais dokta Samia anatarajiwa kutimiza miaka miwili ya uongozi ifikapo machi 19 mwaka huu huku akionesha mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu .Siasa na Demokrasia