Mratibu wa Miradi ya Ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na TARURA,Eng. Humphrey Kanyenye amesema zaidi 90% ya Wakazi wanaoishi katika Bonde la Msimbazi Jijini Dar es salaam wamehakikiwa ili kulipwa fidia kwa ajili ya kupisha uboreshaji wa eneo hilo ambalo hukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara.
Akiongea Dar es salaam , Eng. Kanyenye amenukuliwa akisema “Idadi ya Watu ambao tumewabaini wameathiriwa na mradi ni 2,592 ambao wapo kwenye hilo Bonde, hawa ni lazima waondoke katika kuwaondoa tumefata taratibu zote za kisheria ambazo zinatakiwa kufuatwa katika kuhakikisha kwamba hakuna Mtu anaonewa kwa namna yoyote ile”