Kampuni ya ASAS yenye Makao Makuu yake Mjini Iringa ikijishughulisha na uzalishaji wa bidhaa za maziwa, imetoa shilingi milioni 100 kwa Wafanyabiashara wadogowadogo wa Iringa maarufu kama Machinga ili iwasaidie kujenga vibanda vyao vya kufanyia biashara.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni hiyo Salim Abri ASAS ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Wa Iringa (MNEC) ndiye aliyetangaza msaada huo wa fedha.
Akizungumza na Wafanyabiashara hao, Salim amesema katika fedha hizo milioni 50 itatumika katika ujenzi wa Vibanda vya kufanyia biashara na milioni 50 iliyobaki itatumika kama Mtaji kwa Wafanyabiashara hao.