Mradi wa machinjio ya kisasa ya NGULLU HILLS LIMITED uliopo wilaya ya mvomero mikoani Morogoro umetajwa Kuwa mkombozi kwa wafugaji nchini kutokana na uwezo mkubwa wa mradi huo .
Akizungunza mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge Ustawi na maendeleo ya Jamii Mkurugenzi Mkuu mfuko wa Hifadhi ya Jamii Kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA .Hosea Kashimba amesema mradi huo unauwezo wa kuchinja ng’ombe 100 na Mbuzi zaidi ya 1000 kwa siku.
Amesema kuanza kwa mradi huo katika Wilaya hiyo umekua Mkombozi kwa wafugaji wa mkoa na nchi Kwa ujumla kutokana na watu kuuza mifugo yao Kwa bei nzuri na yenye manufaa.
Kashimba anasema licha ya kutoa fursa kwa wafugaji lakini pia mradi unauwezo wa kuajili wafanyakazi zaidi ya 2000 wakiwemo wamuda na wakudumu hivyo Wananchi wataongeza uchumi wao.
Aidha Kashimba anasema nyama inayozalishwa katika kiwanda hicho asilimia 20 inauzwa nchini huku asilimia 80 inauzwa nje ya nchi hususani nchi za falme za kiarabu na kuongeza pato la taifa Kupitia fedha za kigeni.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Fatma Taufiq amepongeza jitihada za Serikali Kwa kuwainua Wafugaji Kwa ujenzi machinjio hayo ya kisasa na kuahidi Kusaidiana na Serikali kutatua changamoto zinazozikabili Machinjio hayo ikiwemo wingi wa kodi.
Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu,kazi,ajira,vijana na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako ameishukuru kamati hiyo kufika katika mradi huo na kufamu jitihada za serikali ya awamu ya Sita
Amesema Mradi huo wa uwekezaji unafanywa na PSSSF na wabia wenza, Kampuni ya Eclipse Investiment LLC na Kampuni ya Busara Investment LLP ni wa kupongezwa kwani licha ya kwamba kiwanda kipo kwenye majaribio tayari fursa zimeanza kufunguliwa kwa
wafugaji na Vijana.