Katika Kutimiza kwa miaka miwili ya Uongozi wa awamu ya sita iliyochini ya Rais Samia Suluhu Hassan watu mbalimbali wamejitokeza na kumpokezi kwa yale anayoendelea kuyasimamia na kuyatekeleza katika Taifa.
Miongoni mwa waliofunguka kupitia Millardayo.com ni Ahmed Asas ambae ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Maziwa nchini kijulikanacho kama Asas.
‘Kwanza Kabisa ningetumia fursa hii ya kipekee kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kutimiza miaka miwili ya Uongozi hii ni hatua kubwa na anatuoa majibu kwamba Wanawake wanaweza sana hususani kwenye masuala ya Uongozi na hakuna chakuficha amekuwa mstari wa mbele juu ya Maendeleo ya Nchi Safari za hapa pale lengo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na maendeleo makubwa”- Ahmed Asas
“Kingine ni ameboresha Mazingira ya Uwekezaji nchini na kuifanya Tanzania kuwa sehemu salama na sahihi kwa Uwekezaji, hivyo namtakia kila la kheri katika Uongozi wake pamoja na Serikali yake yenye watumishi wanaomsaidia kuyafanya yale yenye kuleta Maendeleo katika Taifa letu, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania“- Ahmed Asas
Aidha pia Mkurugenzi huyo kupitia ukurasa wake wa twitter alipost picha ya bango lililokuwa katika Uwanja wa Uhuru leo Machi 19, 2023 zilipofanya shughuli za Kilele cha Miaka miwili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.